Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
Wameyasema hayo wakati wa wakikabidhiana juzuu ya vitabu vinavyoelezea historia ya SADC ambapo bei kubwa ya vitabu pamoja na lugha ya uandishi inayotumika imetajwa kuwa ni sababu isiyowavutia Watanzania kuwa na mwamko wa kununua na kusoma vitabu licha ya mwamko wa Viongozi na watu wengine mashuhuri wa kuandika vitabu vya historia.
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC ilianzisha mradi wa kuandika na kuchapisha historia ya Jumuiya hiyo ili kuwafanya wananchi wan chi wanachama kufahamu historia ya Jumuiya hiyo.