Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakifungua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Barabara hizo za juu za ngazi tatu (Interchange), itagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 188.71 na itajengwa kwa muda wa miaka 3 na kuhusisha barabara za Nelson Mandela na Sam Nujoma ambapo takribani magari elfu 60 ambayo yatatumia barabara hizo kwa siku na kuwa mwarobaini wa msongamano wa magari katika makutano ya eneo la Ubungo.
Akihutubia katika uzinduzi huo, Rais Dkt. Magufuli amesema serikali yake inalenga kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji na kuchochea mapinduzi ya viwanda na kuweka wazi miradi mingi ya ujenzi wa barabara ambayo analenga kuijenga hivi karibuni na kuiweka Tanzania kwenye nchi ya uchumi wa kati.
Magufuli katika mazunzumzo Ikulu jijini Dar es salaam na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kabla ya kwenda kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017
Kwa upande wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt .Jim Yong Kim amesema, hatua hii ni ya kupeleka faida kwa jamii na kuchochea maendeleo yao, na kwamba Benki hiyo haiungi mkono miradi ya kizembe akitolea mfano ubinafsishaji ambao uliwahi kuleta hasara kwa jamii lakini sasa wanawezesha serikali kwa kutelekeza vipaumbele vya maendeleo na kuahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka wakandarasi waliopewa tenda ya kujenga barabara hizo kutoa kipaumbele kwa watanzania kupata ajira katika ujenzi wa mradi huo, wenye lengo la kurahisisha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam.
Magufuli na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakiwa wamepanda basi la mwendokasi huku wakibadilishana mawazo wakielekea Ubungo kuweka jiwe la Msing la ujenzi wa barabara za juu (Interchange) kwenye makutano ya Ubungo March 20,2017