Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi alipokutana na makamishna wa wizara hiyo na wananchi waliofika wizarani hapo kutoa malalamiko yao yanayowakuta pindi wanapohitaji utatuzi wa migogoro ya ardhi.
Amesema wizara hiyo kuanzia mwezi wa kwanza wanaanza kuhakiki umiliki wa ardhi nchini hasa zile za vijijini na kubaini wanaokwepa kulipa kodi na watayataifisha mashamba ambayo yameshindwa kuendelezwa kwa ajili ya uendelezwaji wa ardhi hiyo nchini.
Aidha katika hatua nyingine amesema kwa wale waliojenga katika maeneo yasiyoruhusiwa tayari wameanza kuweka alama mpya za kutambua maeneo hayo kwa ajili ya ubomoaji utakaoanza tena tarehe 5 mwezi wa kwanza.