Jumatatu , 13th Jul , 2015

Tanzania imeporomoka hadi nafasi ya tatu kwa uzalishaji wa zao la korosho kwa nchi za Afrika kutokana na kukosa viwanda vya kubangulia zao hilo.

Wakina mama wajasiriamali wakiwa wanauza Korosho katika kituo kikubwa cha mabasi yaendayo Mikoani Mkoani Lindi

Kwa mujibu wa ANSAF Tanzania inazalisha korosho zenye ubora wa hali ya juu na wanunuzi wake wako tayari kuzinunua zikiwa zimebanguliwa lakini ujenzi wa viwanda umekua kikwazo kikubwa.

Hali hiyo inakadiriwa kuipotezea Tanzania mapato ya dola za Marekani 110 kila mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Jukwaa la Taasisi za Kilimo ANSAF ya Mwaka 2008 na nafasi ya kwanza inashikiliwa na Ivory Coast.

Aidha ripoti hiyo inaeleza changamoto nyingine inayoyakabili maendeleo ya zao la korosho nchini ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa kutosha huku ikikadiriwa kuwa wilaya 45 zinazojishughulisha na kilimo cha korosho.