Jumatano , 8th Mar , 2017

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Ili kufikia Tanzania ya viwanda nchi inahitaji kuongeza kasi ya kuhakikisha wanawake wanawezeshwa kiuchumi, wanashiriki katika ajira na kukomesha ukatili dhidi yao

Waziri Ummy Mwalimu

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Singida ambapo amesema katika kutekeleza kauli mbiu ya "Tanzania ya Viwanda: Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi" ni lazma kuwekeza katika shughuli zitakazowezesha ushiriki kamili wa wanawake katika shughuli za kiuchumi.

Aidha Waziri Ummy, ameiagiza Halmashauri ya Singida Manispaa kutoa asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kabla ya mwaka wa fedha 2016/2017 kuisha pamoja na kuahidi kufungua dirisha la Benki ya Wanawake katika Mkoa wa Singida ndani ya miezi sita ijayo.

Amesema kuwa ni haki ya mtoto wa kike ni kusoma siyo kuolewa na kuongeza kuwa nchi haiwezi kujenga uchumi wa Tanzania ya viwanda ikiwa asilimia 37 ya watoto wameolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.