Jumatatu , 3rd Jan , 2022

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan, na Watanzania kijumla kufuatia video clip zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha yeye akikashifu mikopo iliyochukuliwa na serikali ya wamu ya sita.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 3, 2022, jijini Dodoma, wakati akitolea ufafanuzi na usahihi wa video zile kwa kueleza kwamba hakuzumgumza hivyo, bali waliosambaza walikata vipande vyao na kuviunganisha hali iliyoleta mjadala mkubwa nchini.

"Niwahakikishie mimi ni yuleyule uimara wangu uko palepale, kwa wale waliorusha matusi tuwasamehe bure, wengine watoto wadogo na ili twende ndiyo maana nimebeba yote na kusema, nimekosa mimi, nimekosa sana, Mungu anisamehe, Watanzania nisameheni," amesema Spika Ndugai

Tazama video yote hapa