Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Spika awapa mbinu CHADEMA ili awafukuze akina Mdee

Jumatatu , 3rd Mei , 2021

Spika wa Bunge Job Ndugai, amemuagiza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika, kuandika barua ambayo ataambatanisha na katiba ya chama chake pamoja na muhtasari wa kikao kilichofanya maamuzi ya kuwafukuza uanachama wabunge 19 wa chama hicho.

kushoto ni Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika na kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai

Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 3, 2021, Bungeni Dodoma, hii ni baada ya uwepo wa malalamiko kutoka kwa viongozi wa chama hicho wakimtuhumu Spika Ndugai kutozingatia katiba kwa kuendelea kukaa Bungeni na wabunge wasiokuwa na sifa za ubunge.

"Aandike barua aambatanishe na katiba ya chama chake, aniambatanishie na muhtasari wa hicho kikao kilichofanya hayo maamuzi, inawezekana huyo Katibu Mkuu kaamka tu kaandika halafu na mimi nakurupuka nachukua hatua, nitakua ni Spika au kitu cha ajabu, hivyo andika ili ile barua niwape watalam waangalie, halafu namuuliza msajili wa vyama hawa wajumbe walioorodheshwa ndiyo wajumbe halisi?", amesema Spika Ndugai

"Pia naangalia kwenye muhtasari ule je hawa wabunge wanaotuhumiwa kufukuzwa walipata nafasi hata ya kujieleza na walisikilizwa?, nifukuze watu ambao hawakusikilizwa popote, yaani mbunge hujawahi kusikilizwa wanaandika tu fukuza hawa, viko vyama vimejaa mfumo dume, kundi la wanaume wamekaa wanafukuza wanawake 19 kwa mpigo hata kama barua hiyo inatoka CCM lazima nitawaambia 'stop' kwanza taratibu", ameongeza Spika Ndugai.

Novemba 25, 2020, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiliwafukuza uanachama wabunge wake 19, akiwemo Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Tunza Malapo, Salome Makamba na wengineo kwa madai ya kwamba ni wasaliti baada ya kwenda kula kiapo Bungeni cha kuwa wabunge wa viti maalum kinyume na makubaliano ya chama chao.

HABARI ZAIDI

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi