kwani alikuwa amepoteza simu yake.
Chin Bees ameiambia eNEWZ kwamba picha iliyosambaa mitandaoni kweli ilikuwepo kwenye simu yake na huyo mwanamke aliwahi kuwa mpenzi wake lakini hakufanya kusudi kuziweka mitandaoni kama jinsi ambavyo watu walivyoanza kumshtumu na kumwambia anatafuta kiki.
"Hiyo picha iloyosambaa kwanza sijajua ni nani aliyeisambaza kiukweli ila sio mimi na huyo dada sipo nae tena kwenye mahusiano, na hayupo hata Tanzania. Lakini ninachofahamu nilipoteza simu yangu muda kidogo nilikuwa kwenye bata moja hivi. Mimi nimefanya kazi zangu za muziki mpaka leo sijatumia kiki sasa kwanini ijekuwa leo" Chin Bees.
Pamoja na hayo Chin Bees amesema kwamba baada ya kutumiwa picha hizo alilazimika kumtafuta mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu kusambaza picha hizo lakini pia alikanusha.
Hii ni skendo ya kwanza kwa Chin Bees kuanikwa mitandaoni kwa kusambaa picha zake za utupu akiwa na mwanamke tangu kuanza safari yake ya muziki.