Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Akizungumza mjini Mtwara katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa, Magufuli amesema ahadi hiyo itatekelezwa na itakuwa ni haki ya kila mwananchi na kwamba hakutakuwa na ubaguzi kwa kuangalia vyama vya kisiasa, dini wala kabila.
Aidha, amesema kuanzia mwakani kutakuwa na fedha za mikopo kiasi cha sh. Milioni 50 zitakazotolewa kwa akina mama na vijana kuanzia ngazi za mitaa, vijiji na kata, ambapo lengo likiwa ni kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wananchi wote.
Aidha Mh. Magufuli amesema kuwa serikali atakayounda itawawezesha wazawa na wageni kuwekeza kiviwanda hasa katika mkoa wa Mtwara ambao una gesi asili ambayo inaweza kuendesha kiwanda chochote duniani.
Aidha serikali ya uchumi na viwanda itatatua tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa kwa karibu asilimia 40 kutokana na sekya hiyo ya viwanda kutengeneza ajira nyingi zaidi.