Mwenyekiti wa baraza la chuo cha ualimu Veta Prof. Elifasi Bisanda
Mwenyekiti wa baraza la chuo cha ualimu Veta Prof. Elifasi Bisanda amesema wao kama wadau watashirii kikamilifu katika kutoa maoni ya kuhakikisha elimu ya ufundi inatolewa bure kama inavyotarajiwa kufanyika kwenye elimu ya msingi na sekondari ili kutengeneza wataalamu wengi wenye ujuzi na ubunifu wanaoweza kujiajiri na kukabiliana na changamoto ya umaskini.
Kwa Upande wake Prof,Idrisa Mshoro ameahidi watasimamia kikamilifu na kuendeleza ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyuo vyote vya ufundi ili kukabiliana na changamoto hiyo na nyingine zilizopo sambamba na kuvifanyia upya usajili vyuo hivyo
Nae Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe ametoa wito kwa wahitimu wa elimu hiyo kujitahdi kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu pamoja na kuwa na weledi wawapo makazini.