Jumatatu , 15th Nov , 2021

Mtaalam wa saikolojia Jiwa Hassan, amesema miongoni mwa sababu zinazopelekea wazazi ama walezi kuwafanyia mateso na pengine kuwachoma moto ama kuwakata mikono watoto inasababishwa na changamoto za mahusiano, kiuchumi na kisaikolojia.

Mtaalam wa saikolojia Jiwa Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 15, 2021, kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio ambao ameshauri kwamba mzazi anapoona hana mahusiano mazuri na mzazi mwenzake ni vyema akatafuta njia ya kutatua changamoto hiyo kuliko hasira zake kuzimalizia kwa mtoto.

"Changamoto kubwa ninayoiona ni ya kisaikolojia mtu anakuwa na maumiviu ambayo hayajapata utatuzi, kwahiyo hasira na msongo wa mawazo anaumalizia kwa mtoto, hivyo unapoona una changamoto hizo ni vyema ukatafuta ushauri kwa sababu unayemuadhibu ama kumuumiza hatumii fikra kama zako bado ni mtoto mdogo," amesema Jiwa Hassan.