Jumanne , 24th Jan , 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi wa nafasi za Viongozi watano

Viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo
1. Bw. Reuben Ndiza Mune, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali;
2. Bw. Msongela Nitu Palela, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mara.
3. Bw. Michael Augustino Matomora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida.
4. Bw. Linno Pius Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga pamoja na
5. Bw. Sunday Deogratius Ndori, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe.
Utenguzi huu ulianza tarehe 22 Januari, 2023.