Ijumaa , 24th Jun , 2016

Rais Barack Obama ameongea kwa njia ya simu na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana na kuahidi serikali yake kuisaidia Kenya ili kuhakikisha mahitaji ya wakimbizi na jamii zinazoishi karibu na wakimbizi yanatimizwa.

Katika mazungumzo hayo Rais Obama amerejea kushukuru ushirikiano imara uliopo baina ya Kenya na Marekani katika masuala mbalimbali, ikiwemo kupambana na ugaidi na kupongeza hatua zilizofikiwa na Kenya katika kulinda usalama.

Kwa mujibu wa taarifa za mazungumzo hayo zilizotolewa na Ikulu ya Marekani, imesema kuwa viongozi hao wawili pia walizungumzia changamoto ambazo Kenya inakabiliana nazo kwa kuwapokea mamia kwa maelfu ya wakimbizi kwa zaidi ya miongo miwili sasa.