Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, amesema wizara hiyo imeanza kufanya mageuzi makubwa kwa taaasisi zake kutoka katika mfumo wa uendeshaji wa kiraia na kuwa wa kijeshi ili kudhibiti vitendo vya Kijangili.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe,

Waziri Maghembe amesema hao wakati akifungua mkutano wa watendaji wakuu wa wizara hiyo na taasisi zake mjini Morogoro unaohusu hali ya uhifadhi za changamoto zake.

Waziri Maghembe ameongeza kuwa kati ya Changamoto zinazoikabili sekta hiyo ni pamoja na baadhi ya viongozi wa hifadhi kushirikiana na wahalifu kuhujumu maliasili za taifa katika maeneo yao.

Aidha amesema kati ya mabadiliko watakayofanya ni pamoja na kuibadilisha TFS kuwa Mamlaka ya misitu pamoja na kupewa hadhi ya jeshi badala kuwa Wakala wa misitu kama ilivyosasa.

Aidha amesema kuwa Wizara hiyo haitawavumilia raia watakaovamia hifadhi kwa kuanzisha kilimo pamoja na kujenga na kuongeza kuwa kwa waliopo sa hivi wataondolewa kwa utaratibu maalum.