Alhamisi , 18th Feb , 2016

Wizara ya Mambo ya ndani kupitia jeshi la polisi wameanzisha mpango maalum wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaoratibiwa na mpango wa matokeo makubwa sasa BRN.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu

Akiongea mara baada ya kusainia makubaliano ya utekelezaji na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Ernest Mangu, Waziri wa Mambo ya ndani Mhe, Charles Kitangwa ameutaka uongozi wa jeshi la polisi kufanya utekelezaji wa mpango huo kwa Uhakika.

Naye IGP amesema wamejipanga vyema kuhakisha kuwa wanatekeleza mpango huo na kwa kuanza wataanza na wilaya ya Kinondoni kwa sababu ndiyo inayongoza kwa matukio ya kihalifu.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRN Bw Omari Isa amesema kabla ya kupatikana kwa mpango huo maafisa wa polisi na viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa walikaa chini na kukubaliana ni mambo gani ya msingi ambayo watatakiwa kuyafanyia kazi na ni kwa namna gani.