Waziri Mwigulu amerejea matukio ambayo hutokea kwa kuanzishwa na viongozi wa siasa na madhara yake baada ya kutotii amri za polisi huwapata wafuasi wao huku viongozi hao wakizidi kuwepo salama bila tatizo.
Waziri ameyasema hayo kufuatia swali la Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga aliyetaka kujua ni hatua gani serikali itachukua kwa viongozi wa siasa wanaosababisha vurugu pia kufanya uchochezi.
Waziri Mwingulu akijibu swali hilo amesisitiza kwamba ‘’Ikitokea uchochezi wowote tutahangaika na kiongozi aliyesababisha tatizo hilo, tataangaika na mzizi wa tatizo.
Aidha Waziri Mwigulu amesema kwamba taarifa za upande wa upinzani kwamba serikali inaendeshwa kimabavu ni za uongo kwani ingekuwa ni udikteta hata hiyo nafasi ya kusema udikteta isingekuwepo.
Waziri ametoa wito kwamba serikali haibagui mtanzania yeyote kwa chama, kabila, rangi au dini yake bali serikali inaheshimu kila mtu kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



