
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadik
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadik ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga matokeo ya ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya Kaskazini yaliyofanyika mjini Moshi na kutanguliwa na maandamano ya wanaharakati kutoka mikoa Kilimanjaro,Manyara ,Arusha na Tanga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa siku 16 za kupinga ukatili Bi Elizabeth Mushi amesema kwa sasa matukio ya ukatili yameongezeka zaidi kwa mtoto kutokana na imani za ushirikina.
Nae Mwenyekiti wa shule ya Polisi Moshi, Afande Theresia Nyangasa amesema kutokana na kuongezeko la vitendo vya ukatili katika jamii, shule hiyo imeanzisha mtaala wa kutoa elimu kwa askari Polisi wote ili kuchukua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili kwenye maeneo yao ya kazi.
________________
Kumpigia KURA msanii unayempenda kwenye #EATVAwards Bofya hapa https://www.eatv.tv/awards