Msanii na Mbunge wa Jimbo la Muheza Mwana Fa
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.
Mwana Fa anaungana na wasanii wengine ambao waliingia Bungeni kama Joseph Mbilinyi aliyeshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini na Joseph Haule 'Prof Jay' aliyeshindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mikumi.
Watu wengi wamempongeza Mwana Fa kwa matokeo hayo akiwemo mtu wake wa karibu na msanii AY ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa "Ni Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma 'Mwana Fa' kwenye moja na mbili hongera, hatimae ndoto yako ya muda mrefu ya kuwatumikia ndugu zako wa Muheza, kila la kheri mwanangu maana nakuaminia kwenye mipango ya kimaendeleo, Mungu ni mwema sana sasa kazi ianze"