Asilimia kubwa ya vijana wasomi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatumia muda mwingi kutumia mitandao ya mawasiliano kwa mambo yasiyo na tija jambo linaloanza kuleta hofu ya kundi hilo kushindwa kusaidia kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayozikabili nchi.
Akizungumza baada ya kukutana na vijana kutoka taasisi mbalimbali za nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katibu mkuu wa jumuiya hiyo Dr. Richard Sezbera amesema inasikitisha kuona vijana wengi wanatumia fursa hiyo kwa mambo ambayo hayawasaidii wao wenyewe wakati yapo matatizo mengi ambayo wangeweza kusaidia.
Akizufungua kongamano la vijana hao linalofanyika Arusha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari Prf Elisante Olle Gabrilel amesema kuna haja ya nchi wanachama kufanya kazi ziada ya kuwasaidia vijana kujitambua na kujua nafasi na fursa walizonazo kujiwezesha wao wenyewe na nchi zao.
Nao baadhi ya vijana wamesema tatizo kubwa lipo katika mifumo isiyo rafiki jambo ambalo lisiporekebieshwa matatizo yanayolalamikiwa sasa yataendelea kuwepo.