
Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe.
Mwambe ameyabainisha hayo alipofanya mahojiano maalum na EATV&EA Radio Digital, na kuongeza kuwa kwa sasa chama hicho hakina budi kujikita katika kuboresha ajenda zake, badala ya kuendelea kuhangaika na mambo mengine.
"CHADEMA watafute ajenda kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ujao sasa hivi hawana ajenda ndiyo kitu ambacho hata mimi kiliniondoa huko kwasababu sijaona ajenda inayotufanya tuende kwa wananchi kuomba kura, sasa hivi wamesha-shift kwenye mambo mengine yote wamebaki kulalama tu ooh mwambe amerudi Bungeni" amesema Mwambe.
Hivi karibuni Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, alieleza kutoitambua barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika ya kulieleza Bunge kuwa lisimtambue tena Cecil Mwambe, kwa kuwa alishajiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama, badala yake Spika Ndugai alimtaka Mbunge huyo kurejea Bungeni.