Jumapili , 11th Feb , 2018

Mgombea Ubunge  wa jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu asesema kwamba hoja ya Uzanzibar inayokuzwa na wapinzani wake kwenye siasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi si jambo jema na haifai kuingia kwenye mjadala kwani inaweza kulipasua Taifa.

Taifa

Akizungumza na www.eatv.tv kuhuhusu tuhuma za U-zanzibar dhidi yake, amesema kwamba anajua kwamba wakati wa vita zinatumika silaha mbalimbali lakini ni vema kwenye hili la la kuleta Utanganyika na U-zanzibar likatumiwa kwa tahadhari ili lisije kuleta madhara.

Akiweka wazi utambulisho wake wa Uzaa, ndg Mwalimu amesema kwamba hajawahi kuuficha utambulisho wake wa kwamba yeye ni ni mzaliwa wa Zanzibar na wala haoni kama ni jambo la ajabu.

"Sifa kubwa ya kuwa mgombea wa ubunge ni uwe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hapo ikimaanisha Tanganyika na Zanzibar. Sasa kama chokochoko hizo zimeanza basi watuambie kwamba Zanzibar nchi yenu hii hapa na Tanganyika tuione ili wazanzibar wawe wanagombea Zanzibar na Watanganyika wagombee bara. Mimi ni Mzanzibar na wala hilo siyo jambo la ajabu" Mwalimu

Hata hivyo Ndg. Mwalimu ameshangazwa na hoja hii kunyooshewa vidole kwake na kuhoji au huenda yeye siyo mtoto wa Kigogo wa Serikali au CCM ndiyo maana imeelekezwa kwake na kusema mbona wapo viongozi kibao kama Waziri

Mwinyi na wengineo waliwahi kuwa viongozi bara huku wakiwa na asili ya Zanzibar na wengine wenye asili ya Tanganyika wakiwa viongozi huko Zanzibar.

Msikilize hapa Chini, ndg Salum Mwalimu akifunguka kwa undani zaidi