.jpg?itok=KWQ_Z6aO×tamp=1480325327)
Waziri wa Sheria na Katiba nchini Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe,
Akizungumzia suala hilo Jijini Mbeya, Waziri Mwakyembe ameitaja mikoa ya Iringa na Njombe kuwa ndiyo mikoa iliyofanya vyema katika zoezi hilo la usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano nchini.
Dkt. Mwakyembe amesem a kuwa lengo la serikali mpaka sasa ilikuwa ni kufikia asilimia 75 lakini kwa mkoa wa Mbeya ni asilimia 56 hali inayoashiria juhudi za ziada zinahitajika katika uandikishaji huo.
Waziri Mwakyembe ameongeza kuwa ni aibu kwa mkoa kama huo ambao kiongozi wake ni msimamizi wa suala hilo kuwa nyuma kiasi hicho, hivyo watumishi waliopewa jukumu hilo hawana budi kuongeza juhudi ili kufanikisha zoezi hilo kwa ajili ya maendeleo ya nchi.