Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa huyo alitoa uamuzi huo katika kikao cha dharura cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo Mjini Langambili kwa madai kwamba Mkurugenzi huyo amesababisha migogoro isiyo ya lazima.
Katika Kikao hico madiwani hao walisema kuwa serikali ilitoa kiasi cha fedha sh milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika halmashauri hiyo lakini kazi hiyo haikufanyika wanapohoji na kutoa maamuzi amekuwa hayafanyii kazi kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliamua kuchukua uamuzi wa kumshimamisha Mkurugenzi huyo na baada ya mahojiano ya papo kwa hapo katika kikao hicho na kumteua mtu mwingine wa kusimamia halmashauri hiyo.