
Dkt. Samia ametoa onyo hilo wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu Mkoani humo, alipokuwa anahutubia wananchi katika viwanja vya Hosptali mpya ya Rufaa iliyojengwa eneo la Mitwero, Kata ya Rasbura mjini Lindi.
Amesema kutumia moto kama nyenzo za Kilimo kina athari kubwa,ikiwemo kuchoma miti ya mikorosho na kupunguza uwezo wa kuzalisha mazao ya aina hiyo kwa wingi,pamoja na kuharibu mazingira ya miundombinu nguzo za umeme.
“Ndugu zangu mnapotumia moto usambaa kwenda kudaka na kuunguza miti ya mikorosho na nguzo za umeme na kusababisha hasara kwa Jamii na shirika” Alisema Rais Dkt Samia
Dkt Samia Suluhu Hassani pia ameutaka uongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya,kusimamia kwenye maeneo yao ya kiutawala kuzuia wananchi wasiwe wanachoma moto hovyo,kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha hasara kwa maeneo mengi ya kiutawala zikiwemo taasisi na Jamii.
Kiongozi huyo wa nchi amewahahidi wananchi wa Mkoa huo kuyafanyia kazi changamoto alizopatiwa zikiwemo wanyama waharibifu wa mazao (Tembo) na zile zinazo husu wafugaji na wakulima,baada ya kubaini Mkoa na Wilaya zimeshindwa kuzipatia ufumbuzi wake.
Awali akimkaribisha Rais Dkt. Samia kuhutubia wananchi walioji tokeza,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Umma na Utawala Bora Mohamedi Mchengelwa amewashukuru wananchi kwa mapokezi mazuri yaliyojaa bashasha waliyoyaonyesha kwa kiongozi wa nchi yetu.