Bohari Kuu ya Dawa nchini imeseama tayari imeshasambaza dawa za aina 300 kwenye maduka ya MSD ndani ya hospital za rufaa wanazozihudumia.
Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Laurean Rugambwa akizungumza na EA Radio amesema ifikapo mwezi wa kwanza mwaka 2016 wanatarajia kufikia idadi ya aina 600 ya dawa.
Amesema kuwa bohari kuu ya dawa imeamua kuongeza idadi kubwa ya upatikanaji wa dawa hizo kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya dawa za binadamu nchini na kwamba lengo ni kutoa aina 800 ya dawa hadi kufikia mwisho wa mwaka 2016.
Amewataka waganga wakuu wa hospital za mikoa kuanzisha maduka yao ya dawa ndani ya hospital zao ambayo yatawezesha MSD kusambaza dawa kwa njia rahisi na watanzania kupatiwa huduma ya dawa karibu na eneo wanalopatiwa huduma ya hospitali na kuwapunguzia watanzania gharama ya manunuzi ya dawa kwenye maduka ya watu binafsi.