
Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Kibiti, mkoa wa Pwani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Peter Kubezya wakati wa uhai wake.
Tukio hilo lilitokea jana saa moja usiku katika kizuizi cha kutoza ushuru wa mazao ya misitu eneo la Jaribu Mpakani wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambapo watu wanne wenye silaha walivamia katika kituo hicho na kuwaua wafanyakazi wawili ambao ni Rashid Mgamba, mlinzi wa kituo hicho, na Afisa uvuvi Peter James .
Watu hao pia walimuua kwa kumpiga risasi tumboni mkuu wa upelelezi wilaya ya Kibiti ASP Peter Kubezya , ambaye alikuwa amefika kusaidia akiwa katika opereshen maalumu.
Mara baada ya tukio hilo watu hao walikimbia na kutelekeza piki piki zao mbili pia waliacha kipeperushi kinachosomeka kuwa kupinga uwepo wa kizuizi cha kutoza mazao ya misitu ikiwemo mkaa kwani walidai ni kudhulumu wananchi wabeba mkaa.
Huyu hapa Waziri Mwigulu akizungumza na wakazi wa eneo hilo.......