Jumatatu , 9th Apr , 2018

Mke wa nane wa Mfalme Mswati wa Swaziland Senteni Masango, amejiua Ijumaa ya wiki iliyopita, wa kunywa dawa za vidonge aina ya amytriptyline, ambazo ndizo zilizoondoa uhai wake.

Malkia Senteni Masango wa Swaziland.

Malkia huyo amejiua wiki moja baada ya kuhudhuria mazishi ya dada yake Nombuso Masango, ambapo tetesi zinasema kwamba Mfalme alimkataza kuhudhuria mazishi hayo.

Habari zaidi zinasema kwamba mke huyo ambaye aliolewa mwaka 1999 na kuwa mke wa 8 wa Mfalme Mswati, alikuwa akiishi kwenye kasri ya Kifalme peke yake kwa takriban miaka mitatu, bila kutembelewa na mume wake huyo.

Tayari Malkia huyo wa Swaziland ambaye alikuwa miongoni mwa wake vipenzi wa Mfalme Mswati amezikwa kwenye eneo la kifalme la Swaziland, huku Mfalme Mswati akiendelea kupokea salamu za pole kwa viongozi mbali mbali wa serikai.

Habari zinasema kwamba Mfalme Mswati alishawahi kukimbiwa na wake wawili kwa tuhuma za unyanyasaji, huku wengine akiwapa adhabu kali ikiwemo kutengwa na kasri ya Kifalme.