NAIBU katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa mashambani (Tpawu), John Vahaye.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe, amesema kuwa tukio lililofanywa na polisi mwishoni mwa mwezi uliopita la kupiga wafanyakazi kiwandani hapo lilitokana na taarifa walizo zipata kutoka kwa uongozi wa kiwanda hicho kuwa kutakuwa na vurugu.
Vahaye amesema kuwa alipata taarifa kupitia kwa viongozi wake kuhusiana na tukio hilo na amaamua kuja mkoani Njombe ili kupata ukweli wa tukio hili na kuwa amezungumza na jeshi la pilisi na kuambiwa kuwa kilichofanywa na jeshi hili kilitokana na taarifa zilizo patikana na kutoka kiwandani ya kuwa huenda kungekuwa na machafuko na kuwa waliamua kwenda wakiwa wamejiandaa.
Amesem akuwa uongozi wa Tpawu kiwandani hapo umesema kuwa wafanyakazi hao walikuja kuwandani hapo wakiwa wanajiandaa kwa mkutano wa saa 2:00 asubuhi ambao walikubaliana kufanyika januari 26 katika mkutano wao wa
januari 3 mwaka huu ambapo uongozi ulibadilisha mawazo hayo na kutaka mkutano huo ufanyike siku hiyo majira ya saa 9:00 alasiri.
Vahaye alisema kuwa kwa kile kilicho fanywa na jeshi la polisi hakiwezi kutatua migogoro ya wafanyakazi mahara pa kazi baina yao na uongozi wa sehemu hiyo na kuwa sheria haisemi polisi wahusishwe katika utatuzi wa migogoro.