
Wakizungumza kwa masikitiko makubwa, baadhi ya madereva wamesema tatizo limekuwa kubwa baada ya kuanzishwa kwa faini za papo kwa papo mwezi mmoja uliopita na kwamba adhabu hizo hutozwa hata katika barabara ambazo hazina alama zinazoelekeza kiwango cha mwendokasi.
Baadhi ya barabara ambazo askari wa usalama barabarani hudaiwa kuchukua rushwa ni pamoja na ile ya Nairobi – Thika ambapo imedaiwa kuwa wanausalama hao hujificha porini wakirekodi mwendokasi wa magari na kisha kuwafuata madereva na kuomba rushwa.
________________
Kumpigia KURA msanii unayempenda kwenye #EATVAwards Bofya hapa https://www.eatv.tv/awards