
Mwanajeshi feki Mrisho Ibrahim (aliyevaa sare za JWTZ) akiwa mikononi mwa Polisi
Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe amesema, alichukua nguo hizo ili asilipe nauli katika basi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa kijana huyo alikamatwa akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni, eneo la Kamachumu wilayani Muleba, na kuwa alipohojiwa amekiri kuiba sare za baba mkwe wake, ambaye ni Askari wa JWTZ mkoani Iringa, na kujifanya ni Askari wa Jeshi hilo kikosi cha mizinga mkoani Arusha.
Akieleza sababu ya kufika mkoani Kagera, Kijana Mrisho Ibrahimu amesema, alimfuata mpenzi wake wa kando (mchepuko) ambaye alimpata kupitia mitandao ya kijamii na kuwa alipofika mkoani humo hakubahatika kukutana naye, ndipo alipoanza kufanya utapeli ili apate nauli ya kurudi alipotoka