Jumatano , 13th Mar , 2019

Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) kutoka Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa ametaja sababu za wanawake wengi kutoa rushwa kwenye siasa ni kile alchokidai kuwa wanawake wanatamani kupewa nafasi za uongozi kiurahisi bila ya kupambana.

Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) kutoka Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa.

Jesca ambaye ni Mke wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe David Kafulila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv kwenye mahojiano yake maalum ambapo amesema, "baadhi ya wanawake wanatoa rushwa ya ngono ili wapate uongozi kwa sababu hawana sifa na hawajiamini, kwamba wanaweza kushinda kwenye nafasi hizo."

"Ajabu maeneo mengine licha ya mwanamke kutoa rushwa ya ngono kupata fursa ila wanazikosa kwa sababu mwisho wa siku kiongozi hapimwi kwa ngono bali ni utendaji na uwajibikaji wake." ameongeza Kishoa.

Hivi karibuni akizungumza na www.eatv.tv Mbunge huyo alisema alilazimika kupigania ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 katika jimbo la Iramba Magharibi akiwa na mimba ya miezi 9.