Jumatatu , 9th Sep , 2024

Uongozi wa Yanga Princess umeweka wazi kuwa malengo yao kwa msimu mpya wa mashindano wa 2024-25 ni kushinda ubingwa wa Ligi kuu ya wanawake Tanzania bara na kushiriki kwenye michuano ya klabu bingwa ya wanawake barani Afrika msimu wa 2025-25.

Kibwana Matokeo ni mratibu wa Yanga Princess ameweka wazi sababu zinazowafanya kuweka malengo ya kuwa mabingwa wa Tanzania msimu wa 2024-25 ni usajili bora na muda walioanza maandalizi ya msimu mpya.

“Tumeanza Mazoezi Mapema ya kuhakikisha wachezaji wetu wapya wanaunga mapema na kuzoeana na wenzao “amesema kibwana Matokeo

Kwa upande wa maandalizi ya kimbinu na kiufundi kocha msaidzi wa Yanga Princess Fred Wilfred  ameelezea maandalizi yao kuelekea katika mchezo wao wa ngao ya jamii dhidi ya Simba Queens utaopigwa  Septemba 24 ,2024 katika Uwanja wa KMC Complex .