Jumatatu , 9th Sep , 2024

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amewapiga marufuku watendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wenye tabia ya kuuza siri za wateja na kuwasababishia matatizo.

Dkt.Selemani jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara

Dkt.Jafo ameyasema hayo wakati anaongea na wakurugenzi wa bodi ya  Brela leo jijini dar es salaam na kuwatka kuwa na maadili mema.
"Brela ni taasisi ambayo ina siri za makampuni mengi kwahiyo ikifanya hivyo itaikosesha uaminifu kwa watu ambao wanaiamini hivyo amewataka kuwa na maadili na uaminifu kwenye utendaji wao wa kazi", Dkt.Selemani Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara.
Aidha Dokta jafo amewataka Brela kutokakuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wanapohitaji huduma.
"Tusiwe kikwazo cha kukwamisha biashara, nawataka mtafute kanuni ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo waweze kuingia kwenye mfumo kwa masharti kwa haraka zaidi ili kuwapunguzia usumbufu na tuweze kuwa na wafanyabiashara wengi zaidi", ", Dkt.Selemani Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara.

Kuhusu Hakimiliki, amewataka waimarishe ulinzi wa hatimiliki za watu ili inapotokea imeibiwa mwenye nayo aweze kunufaika.
"Mfano kwenye majina au bunifu muwawekee watanzania mifumo ya kulinda haki miliki bunifu za watu, na kama mtu atauza  basi ni yeye mwenyewe awe ameuza kwa manufaa yake binafsi",  Dkt.Selemani Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara.