Ijumaa , 13th Sep , 2024

Ukuaji wa Teknolojia nchini umeendelea kukua na kusaidiaq vijana wengi kujikwamua kiuchumi hasa katika matumizi ya utumaji na upokeaji wa miamala ya kifedha hali inayosaidia kurahisisha watazania katika kufanya miamala.

Akizungumza leo katika hitimisho la kampeni ya kuhamasisha watanzania kutumia miamala ya kielektroniki kutoka benki ya exim ikifahamika tap tap utoboe mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wakati Andrew Lyimo amesema matumjzi ya teknolojia ya miamala ya kiktroniki imeendelea kukua ambapo katika kipindi cha miezi mitatu  benki hiyo kupitia kampeni yake wateja zaidi ya 200 wamefanya miamala huku ikipngeza wateja zaidi ya 3000.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha masoko stanley cafuamesema kutokna na mafanikip hayo benki hiyo itaendelea kuja na hamasa kwa ajili ya kuhamasisha watanzaniankutumia miamala ya kiektroniki ili kuunga mkono jitihada za serikali za luachana na malipo ya taslimu.

Katika droo ya leo jumla ya washindi 3 wamepatiakana ambapo wawili wameshinda Pikipiki na Bajaji huku mmoja aliyefahamika kwa jina la Goefrey Muganyizi akishinda zawadi ya Gari  kufuatia kufanya miamala mingi zaidi ya 75  katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hiyo ambayo imewezesha washindi zaidi ya 200 kupatikana.