Ijumaa , 13th Sep , 2024

Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Gilbert Masengeli, amehukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani kwa kosa la kutoiheshimu Mahakama.

Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Gilbert Masengeli

Hii ni baada ya kupuuza agizo la mahakama mara 8, Jaji wa Mahakama Kuu, Lawrence Mugambi, hii leo ameamuru Masengeli ajisalimishe kwa Kamishna Mkuu wa Magereza ili kutumikia kifungo hicho.

Jaji Mugambi amesema iwapo Masengeli atashindwa kujisalimisha mwenyewe gerezani, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi lazima achukue hatua kuhakikisha anakamatwa na kufungwa.

Hata hivyo Jaji Mugambi amesema Masengeli huenda akakwepa kutumikia kifungo ikiwa atafikishwa mahakamani ndani ya siku saba zijazo.

Wakati hayo yakijiri Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki, amewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii dhidi ya kutoa taarifa za uongo na za uchochezi kuhusu mkasa wa shule ya Hillside Endarasha, ambapo wanafunzi 21 walipoteza maisha.