Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (mwenye suti) akizungumza bungeni mjini Dodoma.
Mhe. Lugola ametoa kauli hiyo leo bungeni Mjini Dodoma na kusema bajeti ya Tanzania imekuwa ikitegemea bia, soda na kodi ya Payee wanayolipa wafanyakazi, wakati serikali ikisamehe kodi ambayo ingeweza kusaidia upungufu wa fedha uliopo kwenye bajeti ya serikali.
Akitoa mfano Mh. Lugola amesema ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya serikali (CAG) ya mwaka 2013-2014 ilionyesha kuwepo kwa msamaha wa kodi unaofikia shilingi trilioni 1.5, huku bajeti ya mwaka huo ikiwa na upungufu wa shilingi trilioni 1.5, jambo ambalo iwapo misamaha isingetolewa kusingekuwa na upungufu wa fedha katika bajeti na kuondokana na utegemezi.

