Jumatano , 28th Aug , 2024

Wananchi mbalimbali wamejitokeza kushiriki matembezi ya hisani ya kampeni ya Namthamini Nasisimama Naye yenye lengo la kuhamasisha uchangiaji taulo za kike ili kuwasaidia wanafunzi wa kike nchini wasipitie changamoto ya vifaa wakati wa hedhi wakiwa shuleni.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Abdiel Mengi akiongoza matembezi ya hisani yenye lengo la kuhamasisha uchangiaji wa taulo za kike kwaajili ya wanafunzi shuleni.

Matembezi hayo ambayo yameandaliwa na East Africa Television na East Africa Radio kupitia kampeni ya Namthamini Nasimama Naye yamefanyika leo Agosti 25, Makao makuu ya East Africa Television na East Africa Radio Mikocheni, jijini Dar es Salaam ambapo wadau wametoa wito kwa jamii kuchangia na kushiriki masuala ya kijamii.

Wakizungumza baada ya matembezi hayo wadau mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Elimu Tanzania TEA wameeleza kuhusu umuhimu wa jamii kushiriki kuchangia upatikanaji wa taulo za kike kwa wanafunzi nchini.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Abdiel Mengi akiongoza matembezi ya hisani yenye lengo la kuhamasisha uchangiaji wa taulo za kike kwaajili ya wanafunzi shuleni.

''Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), iliona kuna umuhimu wa kushirikiana na Television na East Africa Radio, kuhakikisha inaunga mkono juhudi zao za kumuwezesha binti wa kitanzania aliyekuwa anakosea siku 5 mpaka 7 za masomo kwa sababu ya hedhi , na sisi TEA, tutahakikisha changamoto hiyo inatatuliwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu'', Mwanaisha Chambega - Mkurugenzi huduma za Taasisi TEA

''Katika Shule zitakazopata nafasi zinapata Choo bora vitakavyowawezesha mabinti kubadilisha taulo zao wawapo shuleni bila kukutana na changamoto ya kimazingira'', Eliminatha Pascal - Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Amref Tanzania.

Washiriki mbalimbali wa matembezi ya hisani ya Namthamini

"Sidi Singida Sunflowers tunaahidi kuchangia Taulo za kike kwa shule ambazo zitachaguliwa kutembelewa na kampeni hii kabambe ya kumuwezesha mtoto wa kike ahudhurie masomo yake bila changamoto", Buruan Salim - Mkurugenzi Singida Rafiki Sunflower.

"Total energies tutashirikiana na TEA, kuchangia taulo za kike kwenye shule zote zitakazochaguliwa na kutembeelewa na tutahakikisha mtoto wa kike anabaki kwenye mazingira salama", Faith Mfugale - Mwakilishi Total Energies.

"Kupitia Kampeni hii tutahakikisha kila shule inapata maji safi na salama pamoja na miundombinu yake", Veronica Ussiri - Mwakilishi Sayari Safi.

Washiriki mbalimbali wa matembezi ya hisani ya Namthamini

"Shule zote zitakazotembelewa tutaweka wataalam wetu ka ajili ya kutoa Elimu ya matumizi sahihi ya taulo nza kike na Elimu kuhusu hedhi salama", Japhet Mswaki - Mwakilishi Tanzania save the community.

"Tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kushirikiana na Television na East Africa Radio, kuhakikisha kamopeni hii inafanikiwa kwa asilimia zote", Kassim Juma - Mwakilishi Hisense.

"Nimeona nichangie taulo hizi ili watoto wetu waweze kubaki shuleni kwa siku za hedhi", Joseph Abdallah-Mwenyekiti Mtaa wa Jitegemee mabibo.

Washiriki mbalimbali wa matembezi ya hisani ya Namthamini

"Tumeshiriki katika kutoa huduma ya kwanza kwenye matembezi haya kama kuta morali kwa jamii kuthamini mchango wa mtoto wa kike", Junior Mshitu - Mwakilishi THMS

"Nimetengeneza madirisha ya chuma kwa ajili ya vyoo vitakavyojengwa kwa ajili ya wanafunzi kujitiri", Saidi Abeid - Fundi Kuchomelea.

"Tuliona vema kuungana na wenzetu wa EATV kutoa elimu kwa pamoja kwani hakuna mama ambaye hajapitia kuwa binti na sisi tunaungana nao kuhamasisha jamii kuchangia taulo za kike", Agaton Kigawa - Mwenyekiti Riverside Jogging.

"Wote tunajua dada zetu kuwa wanaingia kwenye siku zao naunga mkono zoezi hili kwa ajili ya dada zetu", Kasius Ndyamkama - Kiongozi Muongoz Fitnes.

Nini hasa kampeni hii imelenga? "Huu ni msimu wa nane wa kampeni hii na tumelenga kusaidia watoto wa kike mashuleni kupata taulo za kike ili waweze kusalia madarasani inapofika kipindi cha hedhi", Najma Paul.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Abdiel Mengi ameeleza jinsi ambavyo IPP imekuwa mstari wa mbele kuthamini mchango wa mwanamke kwenye jamii huku akitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia kufikiwa kwa malengo ya kampeni hiyo.