Jumatatu , 1st Aug , 2016

Katibu wa chama cha wamilikia wa mabasi nchini TABOA bwana Enea Mrutu amesema kituo cha kimataifa cha mabasi Ubungo bado hakijafanyiwa marekebisho yanayostahili ingawa mamlaka husika tayari imepandisha tozo mbalimbali ndani ya kituo hicho.

Bwana Mrutu ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum nakusema kuwa bado kuna changamoto kubwa sana ya miundombinu ambayo sio rafiki kwa watumiaji wa kituo hicho nakusababisha hasara ya uharibifu wa mabasi na vyombo vingine vya usafiri ambavyo vinatumia kituo hicho kwakua vyombo hivyo vinaharibiwa kwa ubovu huo wa miundombinu.

Amesema wanaiomba serikali kukaa kwa pamoja na wadau hao ili waweze kujadiliana maswala mbalimbali ambayo yanaendelea kutokea katika kituo hicho kikubwa cha kimataifa cha usafirishaji ili wapate suluhisho la matatizo hayo.

Kwa upande wao wasafiri na wenyeji wao wameiomba serikali kuhakikisha wanakaa na kutatua matatizo hayo kwa wakati ili kituo hicho kiwe ni sehemu muhimu yakuongeza pato la taifa kwa tozo mbalimbali ambazo zinatolewa kituoni hapo.