Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Burundi ,Intamba mu Rugamba' wakiimba wimbo wa taifa lao kabla ya moja ya mchezo
Timu ya taifa ya Burundi, 'Intamba mu Rugamba' kuwasili April 24 mwaka huu kucheza na timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars, mchezo wa kirafiki utakaopigwa April 26 mwaka huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ukiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Afisa Habari wa Shirikisho la kandanda nchini Tanzania TFF,Boniface Wambura amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea ikiwa ni pamoja na Taifa stars kuendelea na mazoezi pamoja na kuwaalika waamuzi wa mchezo huo wanaotoka nchini Kenya.
Wambura amesema katika mchezo huo hakuna uhakika wa kuwapata wachezaji ThomaS Ulimwengu na Mbwana Samatta wanaocheza TP Mazembe ya DRC na Mwinyi Kazimoto anayekipiga Qatar kutokana na ugumu wa kuwapata wachezaji hao katika michezo isiyotambuliwa na Shirikisho la soka Duniani FIFA.