Alhamisi , 11th Jun , 2026

Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA limetangaza rasmi kuwa mwamuzi kutoka Somalia, Omar Abdulkadir Artan ndiye atakayechezesha mechi ya UEFA Super Cup kati ya Paris Saint-Germain (PSG) na Aston Villa, itakayopigwa mjini Salzburg, Austria.

Hatua hii imekuja kama zawadi na faraja kubwa kwa Artan (34), ambaye ametoka tu kutemwa kwenye orodha ya waamuzi wa Kombe la Dunia 2026 linaloendelea nchini Marekani, Mexico, na Canada.

Mwamuzi huyo, ambaye ni Mwamuzi Bora wa Mwaka wa CAF (2025), aliondolewa mashindanoni baada ya Mamlaka ya Uhamiaji ya Marekani kumnyima visa na kumrudisha uwanja wa ndege wa Miami.