Alhamisi , 29th Jun , 2017

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amesema licha ya upungufu wa chakula uliopo bado  bei ya vyakula nchini hususani mahindi ipo juu na kusema kwamba hakuna njia nyingine ya kupunguza mlipuko wa bei zaidi ya kudhibiti mazao ya chakula kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim

Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge  wa viti maalum Ritha Kabati wa mkoa wa Iringa alipotaka kujua serikali inatoa ufafanuzi gani kuhusiana na utekelezaji wa tamko la kuzuia usafirishaji wa mahindi.

Mhe. Majaliwa amesema endapo patatokea ulazima wa kusafirisha chakula nje ya mipaka ya Tanzania basi ni sharti mahindi yasagwe ndani ili nchi iweze kupata faida.

"Nimeeleza sisi tumedhibiti kutoa mahindi nje bila ya kibali na kama kuna umuhimu wa kuyapeleka mahindi nje basi yasagwe ndani ili upelekwe 'unga' maana ukisaga kuna faida zake, pumba tunazitumia kwa chakula cha mifugo lakini pia mashine zetu tunazo sisitiza viwanda zitapata kazi ya kusaga pamoja na kutoa ajira" alisisitizia Majaliwa.