
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri mkuu ameeleza kuwa sababu ya kufikia uamzi huo ni kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo.
''Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na butura.”
Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo uliopo kwenye eneo ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za magendo zinafanyika na hakuna kiongozi anayechukua hatua licha ya kuwepo kwa viongozi waliopewa dhamana na serikali.
Agizo hilo la Waziri mkuu linakuja siku chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kumwagiza IGP Simon Sirro kuwasimamisha kazi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa, Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kyerwa, Evarist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa Robert Marwa kufuatia tuhuma za kusafirisha Kahawa kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.