
Aliyehukumiwa kifungo cha maisha Jela na Mahakama ya Mafisadi, Ana Moisie raia wa Msumbiji
Kwa mujibu wa mahakama hiyo mtuhumiwa Anna alikutwa na hatia katika shtaka la kukutwa na kilogramu 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.
Mahakama hiyo imeeleza kuwa mshtakiwa amehukumiwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria ya kuzuia, kusababisha na kupambana na dawa za kulevya.
Mahakama hiyo iliyojibebea jina kama 'Mahakama ya Mafisadi', kwenye kesi hiyo iliongozwa na Jaji Lilian Mashaka ambapo upande wa mashtaka ulithibitisha mashtaka hayo pasipo shaka na baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao, Mahakama imeagiza kuteketezwa kwa dawa hizo.