Ijumaa , 25th Mei , 2018

Rais Dk. John Magufuli amewateua Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere kuwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Kupitia taarifa iliyotolewa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Musigwa imesema kuwa kwa kutumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa katiba ya CCM toleo ya mwaka 2017.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi amefanya uteuzi leo tarehe 25 Mei na kuwateua Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere kuwa wajumbe wa NEC”, imesema taarifa

Majina ya wateule hao yatawasilishwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika tarehe 28 mwezi huu.