Jumatatu , 10th Feb , 2025

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Iponyamakalai Kata ya Nyakamwaga Wilaya ya Geita ameuawa na wananchi wenye hasira kali  baada ya kukamatwa na nyama ya Ng’ombe

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Iponyamakalai Kata ya Nyakamwaga Wilaya ya Geita ameuawa na wananchi wenye hasira kali  baada ya kukamatwa na nyama ya Ng’ombe ikiwa imewekwa kwenye mifuko.

Wakizungumzia tukio hilo wakazi wa kijiji hicho wamesema siku za hivi karibuni kulitokea tukio la wizi Ng’ombe  watatu ambapo wawili walirudi na mmoja kukutwa amechinjwa ambapo wakazi wa eneo hilo kwa kushirikiana na polisi jamii walianza kuwafatilia wezi hao baada ya kuwaona walipiga kelele ya mwizi ambapo wezi wengine walikimbia na wakafanikiwa kumkamata mmoja aliyekutwa na Nyama ndipo walipo anza kumshambulia.

Mwenyekiti wa Kijiji cha lponyamakalai, Lucas Buswelu  amesema kipindi cha miezi 4 nyuma, ng'ombe 12 waliibwa ambapo kitendo hicho kinawakosesha amani wakazi wa kijiji hicho na kuwa na hofu na mifugo yao.