
Watu watatu wafariki na wengine wamejeruhiwa kwenye ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Februari 14,2025 katika Mtaa wa Kimara Stop Over.
Baadhi ya mashuhuda wanasema gari hilo lilifeli brake na kukwepa daladala zilizokuwa zimebaki kwenye zebra na kuangukia watu waliokuwa wamesimama pembezoni mwa barabara pamoja na pikipiki 15, zilizokuwa zimeegeshwa kwenye eneo hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema makondakta wa gari lililosababisha ajali wanasema dereva alikuwa anasinzia toka wakiwa Mbezi na wakamwambia asimamishe gari alale lakini dereva akagoma ndio wakajikuta imetokea ajali hiyo.