Jumanne , 11th Feb , 2025

Mtu mmoja amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali kwa kupinduka baada ya dereva wake kuendesha kwa mwendokasi akiwahisha dawa za kulevya aina ya mirungi kwa wateja.

Mirungi iliyokutwa ndani ya gari

Akizungumza jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo SACP George Katabazi amesema gari namba za usajili T403 EFK aina ya Toyota Alphard liliacha njia na kupinduka likiwa mwendokasi.

"Akijua amebeba biashara haramu dereva aliendesha gari lake mwendokasi na kumshinda kisha kupata ajali na kujeruhi mmoja ambaye alipoteza maisha hospitalini, baada ya kukagua tulikuta viroba vya mirungi," amesema SACP Katabazi