
Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez.
Ushirikiano huo umeweza kuwahamasisha vijana katika maeneo ya Arusha, Dodoma, Zanzibar, Kigoma, Mwanza na Simiyu na harakati hizo bado zinaendelea.
Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez, ambaye ni mmoja wa waendesha semina hizo amesema mpaka sasa wamewafikia vijana zaidi ya watu milioni 10 lakini lengo likiwa ni kuwafikia watu milioni 30 hadi kufikia mwaka 2017.
katika mijadala hiyo hususan mkoani Kigoma, wenyeji wamelalama vile ambavyo Umoja wa Mataifa unahudumia zaidi wakimbizi na kusahau wananchi walio kwenye mazingira magumu.