Jumatano , 29th Jun , 2016

Madereva wanaotumia kituo kikubwa cha Mabasi cha jijini Mbeya wametishia kugoma kutoa ushuru,ikiwa serikali itashindwa kutatau changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ambayo imeendelea kuharibika.

Madereva wanaotumia kituo kikubwa cha Mabasi cha jijini Mbeya wametishia kugoma kutoa ushuru,ikiwa serikali itashindwa kutatau changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ambayo imeendelea kuharibika bila serikali kuchukua hatua ya kuikarabati.

Akizungumza na East Afrika Redio, Katibu wa Umoja wa Madereva wanaotumia njia ya Mbeya/Tunduma, Tambiza Chibona
amesema kituo cha Mabasi cha Mbeya kimekuwa kikipokea idadi kubwa ya watu kutoka Mikoa mbalimbali na wale wa nchi jirani.

Amesema licha ya Madereva kuendelea kutoa ushuru kila siku serikali imeshindwa kukarabati Mashimo yaliyopo kituoni hapo pamoja na jengo la wasafiri ambalo limechakaa kwa kiasi kikubwa.