Alhamisi , 1st Dec , 2022

Zoezi la kubomoa vibanda na meza za wamachinga katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, limeanza kufanyika asubuhi ya leo Desemba Mosi, 2022, ambapo meza nyingi zimeonekana zikibomolewa na bidhaa zao kuchukuliwa.

Baadhi ya meza za wamachinga zilizobomolewa Kariakoo

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng'wilabuzu Ludigija, amesema huo ni utekelezaji wa maagizo yake ya kuwaondoa wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi.

"Kariakoo pale kuna maeneo tulikua tumebakiza mtu mmoja mmoja wakaongeza meza na kufanya njia zisipitike, hayo ni matokeo ya maelekezo yangu hatuwezi kuwa tunarudia kusema kitu kile kile maana yake yakitokea majanga magari hayawezi kupita  na kuwa ni shida kubwa," amesema Mkuu wa wilaya ya Ilala